Penati ya Mugalu Yaua Shabiki wa Simba Ruvuma
Shabiki wa Simba, Ally Rashidi Kuntika (71) mkazi wa Namtumbo mkoani Ruvuma alidondoka ghafla na kufariki dunia papohapo, baada ya Chris Mugalu kukosa goli la penati dhidi ya Tanzania Prisons.
Afisa Mtendaji wa Namtumbo, Geofrey Kalikawe amesema marehemu alikutwa na umauti akiwa katika “kibanda umiza alipokuwa akiangalia mpira na inaelezwa kuwa Simba walipopata penati alifurahi sana.
Mugalu alipokosa penati Mzee Kuntika aliinama kwa muda mrefu. Watazamaji waliokuwa wakishangilia walimsogelea ili kumdhihaki ndipo wakadhani amezirai lakini baadae waligundua amefariki dunia.
Mtoto wa marehemu, Barakati Ally Kuntika anaeleza kuwa baba yake alikuwa mpenzi wa timu ya Simba kindakindaki. Kuthibitisha hilo amesema baba yake aliwahi kutoa mbuzi timu ya Simba ilipopita Namtumbo ikielekea Songea.