The House of Favourite Newspapers

Penzi Kabla ya Kifo-21

0

Msichana bilionea, Elizabeth anaamua kumsaidia msichana mdogo, Glory aliyekuwa amepooza mwili mzima. Msaada huo unasababisha kumpenda kaka wa binti huyo. Wanamchukua Glory na kumpeleka nchini India huku kila mmoja akiwa na majonzi tele.

Songa nayo…

“Unasemaje James…”
“Why are you doing this?” (Kwa nini unafanya hivi?) aliuliza huku hofu ikiongezeka.
“Because I love you James, please, don’t ask me such a question, I truly love you,” (Kwa sababu ninakupenda James, tafadhali usiniulize swali kama hilo, nikakupenda mno) alisema Elizabeth.

Hakuwa na jinsi, alijiona akiwa amebanwa kila sehemu, akashindwa kujua ni kitu gani alitakiwa kufanya mahali hapo. Elizabeth alikuwa mtu pekee aliyekuwa akimpenda kutokana na hali aliyokuwa nayo, umaskini mkubwa uliomtesa kwa kipindi kirefu.

Msichana huyo alijitolea kumsaidia mdogo wake, Glory aliyekuwa hoi kitandani. Hakumlipa kitu chochote kile, alikuwa radhi kutoa mamilioni ya shilingi ili mdogo wake awe mzima na kurudi kama zamani, hivyo kukataa kufanya mapenzi na msichana huyo aliona kama lingekuwa tatizo kubwa.

Akajivika ujasiri mkubwa, akamkazia macho zaidi msichana huyo, hofu iliyokuwa moyoni mwake akajaribu kuitoa na kukishika kiuno cha Elizabeth, kilichofuata baada ya hapo ni sauti za mahaba na kelele za kitanda tu.

Huo ukawa mwanzo wa uhusiano wao wa kimapenzi, kufanya mapenzi ikawa sehemu ya maisha yao, mara kwa mara walipotoka hospitalini, kitu cha kwanza kilikuwa kukumbatiana na kuoneshana mahaba ya dhati tu.

“James….”
“Naaam!”
“Nataka unioe….”
“Nikuoe wewe?”
“Ndiyo! Ninataka unioe James…”

James hakuzungumza kitu, alibaki kimya. Kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwake ni kujidharau. Alikuwa maskini mno, hakuona kama alistahili kumuoa msichana mwenye mvuto na mwenye pesa kama Elizabeth.
Aliuliza mara kwa mara kama Elizabeth alimaanisha kile alichokizungumza au alimwambia kama kumfurahisha kwa kipindi hicho.

“Unamaanisha unachoniambia?”
“Hakika! Ninahitaji uwe wangu milele,” alisema Elizabeth.
“Sawa! Hakuna tatizo!”

Hali ya Glory haikubadilika, bado alikuwa kama alivyofika. Madaktari walihangaika mno lakini hakukuwa na chochote kilichobadilika, bado aliendelea kupooza na kulala kitandani tu.
Madaktari walihangaika usiku na mchana, wengine wakashindwa kulala na familia zao kwa ajili yake lakini pamoja na juhudi zote zile, matokeo yake ni kwamba binti huyo mdogo aliendelea kuwa vilevile jambo lililoleta hofu kubwa.

“Nini kinaendelea daktari?’ aliuliza Elizabeth.
“Bado hali ni ngumu, kama inawezekana, inatakiwa apelekwe hospitali nyingine.”
“Ipi?”
“Rechts Der Isar.”

“Ipo wapi?”
“Jijini Munich nchini Ujerumani.”
“Sawa! Hakuna tatizo!”
Hakutaka kumuona Glory akifariki dunia au akiendelea kuugua ugonjwa ule wa kupooza, Elizabeth aliamua kujitoa kwa kuamini kwamba kitu pekee ambacho kingempa furaha mpenzi wake ni kumtibu Glory mpaka pale atakapopona na kurudi kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.

Alijitahidi kwa nguvu zote, walipoambiwa kwamba Glory alitakiwa kupelekwa nchini Ujerumani, hakuwa na jinsi, akaahidi kulipia gharama zote.
Mawasiliano kati ya hospitali hizo mbili yakaanza kufanyika, utaratibu ukaandaliwa tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini humo.

James hakuacha kulia, kila alipokuwa akimwangalia mdogo wake aliyekuwa hoi kitandani moyo wake ulimuuma mno. Kidogo, Glory alipokuwa India aliweza kupata nafuu kwani hata kuzungumza, alijitahidi kufanya hivyo japo kwa sauti ya chini mno.

James akafarijika, akaona kwamba inawezekana mambo yangekwenda kuwa mazuri endapo tu wangekwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu zaidi. Baada ya siku mbili, safari ya kuelekea Ujerumani jijini Munich ikaanza.

Ndani ya ndege, muda wote James alikuwa pembeni ya kitanda alichokuwa mdogo wake. Moyo wake uliumia mno, kila alipokuwa akimwangalia Glory, alisikia kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake.
Elizabeth alikuwa pembeni yake akimfariji tu. Hakukukuwa na mtu mwingine yeyote yule ambaye angeweza kumfariji katika kipindi hicho zaidi yake, hivyo alihakikisha anakuwa naye karibu kila wakati.
“Elizabeth! Hivi Glory atapona kweli?” aliuliza James huku akibubujikwa na machozi.

“Atapona tu! Tumuamini Mungu!” alisema Elizabeth huku akimpigapiga James mgongoni.

Je, nini kitaendelea? Fuatilia wiki ijayo.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW

INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/

TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari

FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers

YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply