The House of Favourite Newspapers

Penzi la Dimpoz, Mchumba’ke Lameguka!

0

maxresdefaultStaa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Dimpoz’ na Zee.

Stori: Boniphace Ngumije, Risasi jumamosi

DAR ES SALAAM: Jambo limezua jambo! Baada ya kuvuja kwa picha zake akiwa na Mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ kitandani, mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Dimpoz’ anayependa atajwe kwa jina moja la Zee, amegombana na staa huyo.

Chanzo makini kilicho karibu na Dimpoz kimeeleza kuwa, mara baada ya habari hiyo kuchapishwa na gazeti hili, Jumamosi iliyopita, penzi la Dimpoz na Zee lilimeguka na hadi sasa hawana mawasiliano mazuri.

ommydimpoznawemasepetu.jpgDimpoz na Wema.

“Yaani gazeti lilipotoka tu, mtoto wa kike kaja juu, amemaindi kwelikweli. Dimpoz kajaribu kumuelewesha kwa kumwambia ni picha za kitambo lakini wapi. Mtoto wa kike kakaza balaa, hivi sasa hawazungumzi kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Mara baada ya ubuyu huo kutua gazetini mwanahabari wetu alimvutia waya Dimpoz, alipopatikana alikiri kutokea kwa ugomvi na mpenzi wake kufuatia kuvuja kwa picha zake na Wema lakini akadai atayaweka sawa mambo.

mchumba wa ommy dimpoz“Yeah ndiyo hivyo bwana, kimenuka kwelikweli lakini naamini yatakwisha si unajua tena picha zenyewe ziliibwa kwenye simu yangu na ni za zamani, najaribu kuzungumza naye naamini atanielewa,” alisema Dimpoz.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply