The House of Favourite Newspapers

Penzi la Lil Wayne, Christina lavunjika nusu

0

Rapa Lil Wayne akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Christina Milian.

New York, Marekani

SIKU chache baada ya kutangaza kuvunja uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa mwaka mmoja, imebainika kuwa rapa Lil Wayne na Christina Milian hawajatengana katika masuala ya kikazi.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa wasanii hao, zimeeleza kuwa uhusiano huo ulivunjika wiki iliyopita lakini bado Christina ataendelea kuwa memba wa lebo ya Young Money ambayo ipo chini ya Lil Wayne.

Hata hivyo hiyo siyo mara ya kwanza kwa mwanamama huyo kutengana na wapenzi wake wa kiume tangu alipotalikiana na aliyekuwa mumewe The Dream.

Leave A Reply