The House of Favourite Newspapers

Penzi Lenye Maumivu-3

0

Shuleni huko, Rahma hakutaka kurudi nyumbani kwani alikuwa na kazi nyingi, lakini kila siku alihakikisha anashinda shuleni hapo akimsubiri mtoto wake.

SONGA NAYO… HAKUTAKA mwalimu ajue kile kilichokuwa ndani ya mwili wa mtoto wake, alisubiri pale alipotaka kujisaidia, yeye ndiye aliyehusika kumpeleka chooni na kumhudumia huko kitu ambacho walimu wote walihisi kwamba mwanamke huyo alikuwa na upendo mkubwa kwa mtoto wake kumbe nyuma ya pazia ni kwamba hakutaka waone kilichokuwa mwilini mwake.

Hadi anafikisha miaka sita na kuanza darasa la kwanza katika shule ya watoto wa matajiri ya St. Marie iliyokuwa Masaki, hakukuwa na mtu yeyote aliyefahamu kile kilichokuwa katika mwili wa mtoto Halima.

Ingawa alikuwa na jinsia mbili, lakini Halima alikuwa mtoto mzuri kwa sura, kila aliyemwangalia alikiri hakuwahikumuona mtoto aliyekuwa na sura nzuri kama Halima.

 

Kutokana na Hawadhi kuwa na asili ya Kiarabu na Rahma kuwa Mswahili, Halima alikuwa Chotara mwenye rangi mchanganyiko, macho ya gololi, sura pana kidogo na lipsi nene.

 

Ingawa alikuwa mtoto mdogo lakini alionekana jinsi alivyokuwa na uzuri wa ajabu ambaye angewatingisha sana wanaume siku za usoni. Ilionekana kabisa kwamba wanaume wengi hapo baadaye wangepigana vikumbo kumgombania msichana huyo kwani alionekana mpole muda wote.

 

Pamoja na hayo, Rahma alikuwa makini na mtoto wake kwani kila siku alikuwa akimpeleka shuleni, hakutaka kumuona Halima akienda chooni na wanafunzi wenzake, alihakikisha anakwenda pekee yake na kujifungia humo. “Mom! Why me?” (mama! Kwa nini mimi?) aliuliza Halima kila siku. “What do you mean my love?” (unamaanisha nini mpenzi wangu?) aliuliza Rahma huku akitabasamu. “Am I a boy or girl?” (mimi ni mvulana au msichana?) “You are a girl, a beautiful one,” (wewe ni msichana, tena yule mrembo kabisa) “You are lying,” (unadanganya) “I am not lying. Just look at you Halima, you are a beautiful girl, just like an angel,” (sidanganyi. Jiangalie Halima,
wewe ni msichana mrembo kama malaika),” alisema Rahma.

Kila alipoulizwa swali na binti yake, uso wake ulionyesha tabasamu lakini moyo wake ulikuwa na maumivu makali. Alijua kwamba kuna siku binti yake angeuliza swali kama hilo, angetaka kujua ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea mwilini mwake.

 

Aliumia mno lakini hakuwa na jinsi, alimwachia Mungu kwani walipata nafasi ya kumfanyia upasuaji ila hawakutaka kufanya hivyo kwa kuogopa kumsababishia matatizo zaidi maishani mwake hivyo wakaamua kuachana na upasuaji huo.

 

“Kwa nini nina jinsia mbili?” aliuliza Halima. “Mwanangu! Ni stori ndefu. Nitakwambia kwa nini ila hakikisha hakuna mtu yeyote anajua kama una jinsia mbili. Umesikia?” aliuliza Rahma. “Ndiyo Mama! Na kama wakiniona?” “Wewe hakikisha huonekani!”

 

“Na nitaolewa?” “Ndiyo! Utaolewa binti yangu. Wewe ni msichana mrembo mno, hakuna mwanaume atakayekuwa radhi kutokukuoa, ni lazima watakufuata na kukuoa, u mzuri sana binti yangu,” alisema Rahma kisha kumkumbatia binti yake.

 

Alijikaza sana lakini Halima alipoelekea chumbani kwake, Rahma alibaki sebuleni huku akilia sana. Hakutarajia kuulizwa maswali kama yale aliyoulizwa na binti yake. Hakunyamaza, hadi mumewe, Hawadhi alipofika nyumbani hapo, bado alikuwa akilia tu kama mtu aliyeumizwa na jambo moja kubwa. Hapo hapo Hawadhi akamfuata na kukaa karibu yake kochini pale. “Kuna nini?” aliuliza.

 

“Halima!” “Amefanya nini?” Rahma hakujibu swali hilo, akamkumbatia mumewe na kuendelea kulia. Alimuonea huruma, alijua ni kwa jinsi gani angepata shida maishani mwake hapo baadaye. Wakati mwingine alitamani kila kitu kilichokuwa kimetokea katika maisha yake na binti yake iwe ndoto moja ya kusisimua ili baada ya muda fulani ashtuke kutoka usingizi.

* * * Maisha ya mtoto wao yaliwaumiza mno, kila siku kwao zilikuwa siku za majonzi, kila walipomwangalia Halima, waliyaona majonzi machoni mwake kitu ambacho kiliendelea kuwaumiza kila siku.

 

Halima akazidi kuwa mrembo, umbo lake la kimisi likaanza kujaa, nyonga zikaanza kuonekana kwa mbali, ingawa alikuwa mtoto mdogo lakini alionyesha dhahiri kuwa atakuwa

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Siku ya Jumatatu.
na umbo zuri siku za mbeleni. Miaka ikakatika, alipoingia darasa la saba, akapevuka, urembo ukaongezeka maradufu huku sauti yake ikiwa nyororo mithili ya ile ya kumtoa nyoka pangoni.

 

Shuleni alikuwa gumzo, wanafunzi wengi walimpenda, wengi wakatamani kulala naye kitanda kimoja, lakini kwa Halima jambo hilo lilikuwa gumu mno kutokea. Alikuwa mkimya, hakutaka kuwa muongeaji sana kama wasichana wengine.

 

Hilo liliwapa wavulana wakati mgumu kumzoea na hata kumwambia hisia za mioyo yao kwani ukimya wake, aina ya maisha aliyochagua kuishi vilikuwa vitu vilivyowanyima fursa wavulana hao kumwambia kwamba walikuwa wakimpenda. Hakuwa na akili nyingi darasani, alikuwa na uwezo wa kawaida, upole wake ukawafanya watu wengi kupenda kuongea naye, lakini muonekano wake tu haukuwa wa kuwakaribisha watu hao kuzungumza nao, hasa wanafunzi wenzake.

Leave A Reply