The House of Favourite Newspapers

Pepe atuma salamu Wanaomponda

NICOLAS Pepe, kiungo mshambuliaji wa Arsenal ametuma salamu kwa wanaoponda kiwango chake baada ya kusema kuwa, muda si mrefu atarejea kwenye ubora wake kama zamani licha ya hivi sasa kupitia kwenye kipindi kigumu.

 

Pepe aliyesajiliwa kwa paundi milioni 72 ikiwa ni usajili ghali ndani ya kikosi hicho, amefanikiwa kufunga bao moja pekee tangu ajiunge na timu hiyo huku akicheza mechi saba za Ligi Kuu England ambapo amekuwa akitupiwa maneno mengi na mashabiki wa timu hiyo kuwa hana msaada wowote.

 

Akizungumzia kiwango chake, Pepe amesema: “Mwanzo wangu hapa siyo mzuri tofauti na nilivyokuwa Lille. Naamini kiwango changu kitarudi kama zamani, sina hofu juu ya hilo licha ya watu kuwa na wasiwasi na mimi. Wanaonisema vibaya acha waseme, sijali.”

LONDON, ENGLAND

Comments are closed.