Pete ya uchumba ya Bela yazua utata

Gladness Mallya

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu msanii wa filamu na muziki, Isabela Mpanda ‘Bela’ avishwe pete ya uchumba na mwandani wake, Luteni Karama, pete hiyo imezua utata baada ya wazazi kuja juu na kudai ni batili.

Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Isabela kilieleza kwamba wazazi wake wamemjia juu na kumweleza kwamba hawatambui uchumba wake na Karama kwani hajawahi kupeleka barua ya posa nyumbani kwao na hawamfahamu zaidi ya kumuona kwenye vyombo vya habari.

Baada ya kupata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Bela ili kuujua ukweli ambapo alikiri kwamba ni kweli Karama alimvisha pete ya uchumba lakini hajawahi kupeleka barua ya posa kwao wala kujitambulisha.

“Niko kwenye wakati mgumu kwani ni miaka 16 sasa niko kwenye uhusiano na Karama na alinifanyia sapraizi ya pete ya uchumba lakini familia imekataa kuutambua uchumba huo kwani hakuwahi kufika kwetu na Karama bado hajafikiria kwenda,” alisema Bela.


Loading...

Toa comment