The House of Favourite Newspapers

Peter Msigwa: Jamani Polisi Msinivizie

0
Mbunge, Mchungaji Peter Msigwa.
MBUNGE wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa amepata taarifa jeshi la polisi linamtafuta na kusema endapo jeshi hilo litamuita kwa kufuata utaratibu basi ataitika wito huo ila si kuviziwa
Msigwa ametoa taarifa hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa toka jana kuwa kiongozi huyo anatafutwa na jeshi hilo akidaiwa kuwa ni mmoja kati ya waliokuwa wakiratibu mkusanyiko ambao ulitakiwa kufanyika jana kumuombea Mbunge Tundu Lissu katika Viwanja vya TIP Sinza, jambo ambalo amepinga na kusema bado yupo nchini Kenya.
“Nimepata taarifa kuwa polisi wamenitafuta toka asubuhi (jana) maeneo ya Sinza, wakisisitiza kuwa nipo hotelini hapo, wakati mimi niko Nairobi.
“Nitaitika wito wa polisi ukiletwa rasmi, sihitaji kuviziwa, +255754360996 mnaweza kunipigia au kunitumia ujumbe mfupi WhatsApp,” alisema Msigwa.
Mbunge huyo bado yupo jijini Nairobi kwenye matibabu ya Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

KIMENUKA! Polisi Walivyowatimua Chadema Kwenye Ibada Ya Lissu

Leave A Reply