The House of Favourite Newspapers

Peter Okoye atumbuiza peke yake, ajipa jina jipya

0

peter-okoye1Peter Okoye.

UVUMI umeenea tangu mwishoni wa wiki iliyopita kwamba mwanamuziki maarufu wa Nigeria, Peter Okoye, wa kundi la Psquare aliyeonekana anatumbuiza peke yake, ni ishara ya mwanzo ya kuvunjika kwa kundi hilo linaloongozwa na mapacha wawili.

Peter, ndugu yake, Paul, alifanya onyesho hilo kwenye klabu moja jijini Abuja, Nigeria, alipopiga wimbo unaoitwa ‘Look into my eyes’ (Tazama machoni mwangu) ambapo watu wengi wanakisia huo ndiyo mwisho wa kundi hilo la waimbaji hao.

peterrrrIsitoshe, Peter Okoye, hivi sasa anatumia jina la Mr P na anaendesha shughuli zake chini ya menejimenti mpya ambapo Aprili 7 mwaka huu atatumbuiza jijini Dubai.

Pamoja na yote hayo, pacha wake, Paul, aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba anatamani mama yao angekuwa hai na kusaidia katika mfarakano huo.

“Natamani ungekuwa hai, na sasa natambua maisha yalivyo bila ya kuwepo mama,” aliandika Paul.
Wakati huohuo, Jude, kaka yao na meneja wao wa zamani, pia aliandika kwenye mtandao huo kuwaomba mashabiki waendelee kutabasamu na bila kujali kitu.

Mashabiki waliozagaa duniani kote wanawaombea Psquare wamalize tofauti zao na waendelee na muziki wao.

Leave A Reply