The House of Favourite Newspapers

PETIT AFUNGUKIA MADAI YA KUTEMBEA NA MTOTO WA GARDNER

Hemed Manungwa ‘Petit Man’

MENEJA wa wasanii mbalimbali Bongo, Hemed Manungwa ‘Petit Man’ amefungukia madai ya kutoka kimapenzi na mtoto wa mtangazaji wa Redio Clouds FM, Gardner Habash, Careen kwa kusema madai hayo hayana ukweli wowote.

Akizungumza na Amani, Petit alisema anashangaa kuona watu wanasambaza umbea mitandaoni kuwa anatembea na Careen, kitu ambacho si cha kweli na binti huyo anamchukulia kama mdogo wake na ni marafiki pia.

“Watu wanasema sana juu yangu na Careen lakini hawaelewi yule ni kama mshikaji lakini kingine ni kama mdogo wangu wa karibu sana hivyo siwezi kuwaziba midomo wanaotaka kuzungumza chochote maana kila mtu amejaliwa mdomo wake wa kusema,” alisema Petit Man

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.