The House of Favourite Newspapers

Petit, Esma mahaba upya!

0

AUNT PETIT IYOBO COOKIE ESMA (2)DADA wa staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul na mumewe, Petit Man wameonesha wako katika mahaba mapya baada ya kipindi cha nyumba kutengana kwa muda.

Esma na mumewe huyo walionekana wako ‘beneti’ kwenye sherehe ya kuzaliwa mtoto wa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel iliyofanyika hivi karibuni Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo muda wote walikuwa katika nyuso za furaha na mtoto wao, Taraj.

 “Naona sasa hivi Esma na Petit Man mapenzi yamerudi upya Mungu awaongoze,” alisikika mdada aliyekuwepo kwenye sherehe hiyo.

Kwa upande wa Petit Man alisema Esma ni mkewe na pia ni mzazi mwenzake  hivyo hawezi kumuacha kirahisi.

Leave A Reply