The House of Favourite Newspapers

Petit Man ajitosa kwa Dada wa Kiba

0

petitMFANYAKAZI wa kampuni inayomilikiwa na Wema Sepetu, Endless Fame, Petit Man Wakuache amenaswa akijiweka karibu na dada wa Ali Kiba, Zabibu Kiba kiasi cha kuzua minong’ono kwamba huenda alikuwa akimtongoza.

Ubuyu huo ulinaswa moja kwa moja ndani ya Ukumbi wa Wema, Kijitonyama jijini Dar ambapo muda mwingi wawili hao walikuwa wakikaa pamoja na baadaye kila walipokwenda, walikwenda pamoja.

Dada wa Kiba alipobanywa na Amani kuhusu ukaribu wao, hakuwa tayari kuungumzia lakini Petit alipoulizwa alitiririka:
“Huyu dada yake na Ali Kiba si unajua tena mjini unaangalia wapi unapenda na hapa ndiyo kwanza najipenyeza.”
Awali, Petit alimuoa dada wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma ambaye alizaa naye mtoto mmoja kisha wakaachana.

Leave A Reply