The House of Favourite Newspapers

Petit Man Nisingeweza Kuachana Mazima na Esma

0

 PENZI la kweli halifi na hata likifa haliozi, haya ndiyo maneno aliyotamka meneja wa wasanii mbalimbali nchini, Ahmed Hashim ‘Petit Man’ ambaye anasema kuwa asingeweza kuachana mazima na mkewe ambaye ni dada wa mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan.

 

Petit Man ambaye hivi karibuni alirudiana na Esma baada ya kuachana kwa muda alisema, mkewe huyo ni mwanamke anayempenda kweli hivyo asingeweza kuachana naye mazima kama ambavyo watu wengi walikuwa wakidhani. Ndiyo maana alihakikisha anaweka mambo sawa na wao wanakuwa tena pamoja.

 

“Esma tayari tumejaaliwa kuwa na mtoto ambaye kiukweli anahitaji malezi ya pande zote mbili, pia ni mwanamke ninayempenda sana.

Hivyo nisingeweza kuachana naye mazima, lakini tunajifunza kutokana na makosa pia ugomvi kwenye mapenzi ni jambo la kawaida tu, ila mwisho wa siku kama mnapendana kweli mnakaa chini na kumaliza tofauti zenu,” alisema Petit Man.

Stori: Memorise Richard

Leave A Reply