The House of Favourite Newspapers

Petit Man: Soon Namzalisha Esma

0

MENEJA wa wasanii mbalimbali wa muziki, Hamad Manungwi ‘Petit Man’ amefunguka kuwa anatarajia kumzalisha mtoto mwingine mkewe Esma Khan ambaye ni dada wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Petit alisema amerudi kwa mkewe kwa kishindo kwa sababu ni mwanamke anayempenda sana, hivyo wao wanapenda familia ndiyo maana wanatarajia kuongeza mtoto mwingine.

 

“Nimerudi kwa mke wangu kipenzi, sifichi nampenda sana sana na nikamwambia hivi karibuni tutaleta kabebi kengine maana mimi na mke wangu tunapenda sana familia maana watoto wetu ndiyo furaha yetu,” alisema Petit ambaye aliachana na mkewe huyo kwa talaka na sasa amerejesha majeshi upya.

 

Leave A Reply