The House of Favourite Newspapers

Petitman Amefulia, Hawezi Kumhudumia Mtoto Wake?

SIKU ya Septemba 23,2019 kwenye kipindi cha Katambuga kinachorushwa na  +255Global Radio, meneja wa wanamuziki, Petitman aka Batikayo,  aliongea mambo  mengi ikiwemo ndoa yake mpya  na mahusiano na mama mtoto wake, Esma, ambaye amemtaja kutokuwa na maelewano naye kiasi cha kumnyima hata uhuru wa kumuona mtoto wao Baby Taraj.

“Natoa kila kitu kuhusu mtoto lakini hivyo sio vitu vya kusema, mimi ninachoumia kama baba nahitaji nafasi yangu kumuona mtoto lakini sipati nafasi hiyo mpaka mtoto akiwa shule au kwa bibi yake Mama Dangote,” alisema akikanusha madai kwamba ameshindwa kumhudumia mwanaye huyo waliyezaa na Esma ambaye ni dada yake nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz..

Batikayo ameyasema hayo baada ya kuulizwa kuhusu uvumi kwamba hana maisha ya kumlea mtoto wake kwa maana  hayuko vizuri kiuchumi hadi ameamua kuoa mwanamke mtu mzima kwa sababu mwanamke huyo ana uwezo mkubwa kipesa.

Akijibu swali  hilo, Petitman amekanusha kutofuata hela kwa mwanamke huyo kwani yeye hajafulia kiasi hicho kwa vile  ofisi yake inamuingiza hela nyingi tu. Pia amemshukuru Mama Dangote kwa mapenzi ambayo amekuwa anamuonyesha tangu siku ya kwanza hadi ndoa yake na Esma ilipovunjika ambapo mama huyo ameendelea upande wake.

Comments are closed.