The House of Favourite Newspapers

Pharrell Williams Anaichukia Mistari Ya Ngoma Zake

MWANAMUZIKI kutoka pande za Marekani, Pharrell William amefunguka kuhusu mistari ya ngoma zake za zamani ilikuwa mibaya hapendezwi nayo tena.

Kupitia Jarida la GQ limefanya mahojiano na pharrell williams amefunguka na kusema amepitia mengi kwenye muziki wake amekosolewa sana baadhi ya mistari yake kwenye nyimbo ya Robin ‘Blurred Lines’ ambayo ilikuwa inawadharirisha wanawake, “Nilizaliwa katika nyakati tofauti ambapo sheria wakati huo ziliruhusu vitu vingi ambavyo kwasasa haviruhusiwi, Najutia sana kutumia ile mistari kwenye wimbo wa Blurred Lines”.
Mwanamuziki Pharrell William amesema kuwa baadhi baadhi ya mistari ya nyimbo zake hawezi kuiimba tena kwasababu hafuraishwi nayo na anaijutia kuiandika.

 

Comments are closed.