PhD ya Baba Levo ya Mchongo?
MWEZI mmoja uliopita, Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Kasheku almaarufu Msukuma alitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Siasa na Uongozi (Honorus Causa in Politics and Leadership) na Chuo cha Academy of Universal Global Peace cha Marekani.
Kwa mujibu wa Msukuma alipewa heshima hiyo kama sehemu ya kutambua mchango wake kwenye siasa na uongozi nchini Tanzania.
Sherehe za kutunukiwa udaktari huo wa heshima kwa Msukuma zilifanyika jijini Dodoma kabla ya kuzua mjadala mzito ikifahamika kwamba yeye ni mwakilishi wa wabunge walioishia darasa la saba.
Awali, Msukuma alitambulika kama darasa la saba, lakini hivi sasa ana PHD ya Heshima.
Tukio kama hilo limejirudia tena kwa msanii Baba Levo au Fundi Majumba kutunukiwa PHD (Shahada ya Udaktari wa Falsafa) ya Heshima.
Baba Levo aliandika; “Uongozi wa Chuo cha Madatari @city_college_mwanza_ campus ulinipatia chetin cha udaktari wa heshima…!!! PHD ya Afya Siasa, Sanaa na Burudani.
“Niseme nashukuru sana kwa heshima waliyonipatia..!! From now call me Doctor..!!”
Baadhi ya watu walipata mshituko mkubwa kama ilivyokuwa wakati wa mlipuko wa mabomu ya Mbagala, maana hawajaamini kilichotokea huku wengi wao wakidai ni mchongo wa kupewa.
STORI; SIFAEL PAUL, DAR