The House of Favourite Newspapers

Pia Wurtzbach ndiye Miss Universe 2015

0

Las Vegas, Marekani
Usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Desemba 21, 2015 katika Ukumbi wa AXIS, Las Vegas, Nevada nchini Marekani, lile shindano kubwa la ulimbwende duniani la Miss Universe, lilitimua vumbi ambapo mrembo kutoka Ufilipino (Philippines), Pia Wurtzbach aliibuka kidedea na kuvalishwa taji hilo.Pilipinas_pia_alonzo_wurtzbach-010 Pia akiwapungia mkono mashabiki baada ya kutangazwa mshindi

Kituko katika fainali hizo, kilikuwa ni pale MC wa shindano hilo, Steve Harvey alipomtangaza kimakosa mshiriki kutoka Colombia, Ariadna Gutiérrez huku mshindi halisi, Pia Wurtzbach akitangazwa kuwa mshindi wa pili. Baada ya kutangazwa, Ariadna alivalishwa taji lakini muda mfupi baadaye, MC huyo aliomba radhi kwamba amesoma vibaya jina la mshindi, hali iliyozua taharuki kubwa ukumbini.pia_alonzo_wurtzbach-001Pia akivalishwa taji

Ikabidi mshindi aliyetangazwa kimakosa, avuliwe taji ndipo mshindi halisi, Pia Wurtzbach alivalishwa upya taji hilo na mrembo aliyekuwa akimaliza muda wake, Paulina Vega wa Colombia. Washindi wengine ni Ariadna Gutiérrez aliyeshika nafasi ya pili (1st Runner-up) na Olivia Jordan wa Marekani aliyeshika nafasi ya tatu (2nd Runner-up).

Tanzania ilikuwa ikiwakilishwa na mrembo Lorraine Marriot ambaye hata hivyo hakufua dafu.

Leave A Reply