Pialali Kuzichapa na Muhindi Bagamoyo
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Shiva Gurgaon raia wa India katika pambano la ubingwa wa International UBO linalotarajia kupigwa Desemba 16, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Travel Lodge, Bagamoyo mkoani Pwani.
Pialali ambaye pia anashikilia Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati ambao aliupata Julai 23, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live kufuatia kumchakaza vikali mpinzani wake, Rigen Champion raia wa DR Congo.
Mbali ya pambano hilo lililoandaliwa na Sharif Promotion ambalo limedhaminiwa na Kinite Castle, Travel Lodge, mapambano mengine ya utangulizi yatakuwa ni kati bondia Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe, dhidi ya Ambukile Chusa (raundi kumi), Saleh Mkalekwa dhidi ya Hamis Ng’onda (raundi nane).
Mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni Bruno Vifua viwili dhidi ya Said Uwigo (raundi nane) wakati Ramadhani Mchongo akitarajia kuzichapa na Twalip Tuwa huku mwanadada, Rehema Nakozi atazitwanga na Happy Daudi (raundi sita) na Pallasoguru Mchalinze dhidi ya Shebi Chui (raundi kumi)
Comments are closed.