The House of Favourite Newspapers

Pichaz: Hapa ni Kisiwani Ambapo Rais Obama na Mkewe Wameenda Mapumziko ‘Kula Bata’

obama-1         obamas-homeRais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle Obama walifika katika kisiwa cha Necker kinachomilikiwa na bilionea wa Uingereza, Sir Richard Branson, Jumatatu hii kwenye mapumziko wanayostahili baada ya kumaliza kipindi chake cha Urais.

obama-3Obama na Michelle waliondoka Washington D.C siku ya Ijumaa mara baada ya kuapishwa kwa Donald Trump. Kabla ya kupanda ndege kwenda mapumzikoni, Rais huyo wa 44 wa Marekani aliwatania waandishi.

obama-4“Michelle na mimi tumetamani kupumzika kwa muda mrefu sana, kwahiyo leo sisemi chochote.”  Hawakupoteza muda baada ya kusema hayo, walipanda ndege yao na kwenda mapumzikoni.

obama-5Kwanza walianzia Palm Springs, California, kwa mapumziko mafupi katika mji wa mapumziko uitwao Rancho Mirage Home unaomilikiwa na James Costos, aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Hispania na Andorra wakati wa utawala wa Obama.

obama-6Baada ya hapo waliekekea Caribbean katika kisiwa binafsi cha Necker.

obama-2Inaelezwa kuwa, kama mmiliki wa kisiwa hicho, bilionea Sir Richard Branson hayupo kisiwani hapo, basi nafasi huwa inakuwa wazi kwa mtu yeyote kukikodi na kwenda kustarehe ama kupumzika.

obama-7Kwa hiyo watu wengi mashuhuri duniani wamekuwa wakivizia kwa kutokuwepo kwa bilionea huyo ili nao wakajivinjari.

obama-8Mastaa kama Mariah Carey, Robert DeNiro, Princess Diana na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela washawahi kwenda mapumzikoni kwenye kisiwa hicho.

obama-9Michelle Obama alipigwa picha akiwa anapanda kwenye ndege Binafsi ya bilionea Richard Branson iliyowapeleka moja kwa moja kisiwani hapo kwa mapumziko yao.

obama-1Bado haijajulikana Obamas na Michelle watakaa kisiwani hapo kwa muda gani.

Tazama video fupi inayoonesha mandhari ya kisiwa hicho:

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.