The House of Favourite Newspapers

PICHA ZA UTUPU NI STAILI ILIYOFELI – TUNDA

0
Tunda Sebastian.

MUUZA nyago machachari Bongo, Tunda Sebastian amewapa makavu mamodo wanaoibuka kwa staili ya kupiga picha za utupu akisema fasheni hiyo hivi sasa imefeli, hivyo ni bora wakitafuta namna nyingine ya kutoka.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Tunda alisema wasichana wanaokuja na kudhani kuwa kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni kutawafanya wawe maarufu, wamechemsha kwa sababu wanachokifanya ni ujinga uliopitiliza.

“Ninachokiona hapo ni upumbavu tu na tamaa ya umaarufu bila kutafakari madhara yake, kifupi watafute plan B maana A imefeli na kuwadhalilisha,”alisema.

STORI: MAYASA MARIWATA| RISASI

Tambwe na Chirwa Waenguliwa Kikosini Yanga

Leave A Reply