PICHAZ: Dogo Mfaume Alivyozikwa Dar
JUZI JUMATANO, Mei 17, 2017 tasnia ya muziki wa Bongo ilikumbwa na msiba mkubwa baada ya kuondokewa na msanii Mfaume Suleiman ‘Dogo Mfaume’ aliepata umaarufu kutokana na wimbo wake wa ‘Kazi ya dukani’, mauti yalimkuta akiwa kwenye hospitali ya taifa Muhimbili akijiandaa kufanyiwa upasuaji kichwani ambapo amezikwa leo Mei 19 katika makaburi ya Chanika jijini Dar es salaam.
Shughuli ya kuuzika mwili wa marehemu Dogo Mfaume imefanyika nyumbani kwao Chanika ambapo amezikwa katika makaburi ya Kwa Mbiki – Chanika jijini Dar es Salaam.
Waathirika wa dawa za kulevya kutoma Pili Foundation (Soba) wakimwombea dua marehemu Dogo Mfaume.