The House of Favourite Newspapers

PICHAZ: Mwili wa Ali Yanga Alivyoagwa Dodoma

0
Ali Yanga enzi za uhai wake.

MWILI wa aliyekuwa shabiki maarufu ya Klabu ya Yanga, Ally Mohammed maarufu kama Ali Yanga jana uliagwa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma na kusafirishwa kwenda kuzikwa kwao mkoani Shinyanga.

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana akiwa na Waziri wa zamani wa Habari na Michezo, Nape Nnauye pamoja na waombolezaji wengine.

Miongoni mwa waliohudhuria tukio hilo la kumuaga Ali, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana na Waziri wa zamani wa Habari na Michezo, Nape Nnauye, mashabiki na wanachama wa Yanga na wapenda soka.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Ali Yanga wakati wa kuagwa.

Ali Yanga alifariki juzi Jumatatu, Mpwapwa, Dodoma kwa ajali ya gari ambapo baada ya kuagwa jana mwili wake ulisafirishwa kwenda kwao Shinyanga kwa mazishi ambayo yanafanyika leo.

Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana akisaini katika kitabu cha wageni msibani hapo.

Simanzi na Vilio Vyatawala Kuagwa kwa Shabiki wa Yanga, Ally Yanga

Leave A Reply