Rais wa Marekani, Donald Trump amewasili nchini Saudi Arabia ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku 9 Barani Asia na Ulaya ambapo Mikataba ya mabilioni ya madola kati ya Marekani na Saudia itatiwa saini leo Jumamosi.
Bwana Trump na mkewe Melania walipokewa na mfalme wa Saudia Salman Jumamosi alfajiri. Swala kuu linalotarajiwa kuzungumziwa kwenye kikao hicho ni vipi kukabliana na itikadi kali zinazosababisha vitendo vya kigaidi.
Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kimataifa kwa rais huyo, pia itashirikisha Israel, Palestina,Ubelgiji,Vatican na Sicily.
Ziara hiyo inajiri wakati ambapo Trump anakabiliwa pigamizi kali nchini mwake kufuatia hatua ya kumfua kazi Mkurugenzi wa Shirika la FBI, James Comey.
Amekosoa vikali uamuzi wa kumteua mtaalam kuchunguza ushawishi wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.
Bwana Trump anaandamana na mwanawe Ivanka, Mshauri wa Ikulu ya White House pamoja na mumewe Jared Kushner ambaye ni mwanachama muhimu wa Baraza la Mawaziri la Rais Trump.
Kama Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusu ziara zao za hivi karibuni nchini Saudia, Trump na Ivanka hawakuvaa hijab.