PIERRE AFUNGUKA KUIBIWA JINA NA DUDU BAYA
JAMAA aliyejizolea umaarufu nchini kwa staili yake ya kuchapa maji, Peter Mollel maarufu kwa jina la Pierre Konki amemuelezea msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ambaye naye anatumia jina hilo akijiita Konki Master jina ambalo yeye ndiye aliyeanza kulitambulisha hapa nchini.
Akizungumza na Showbiz, Pierre alisema yeye haoni ubaya watu kutumia jina lake na kuwataka hata wengine wanaotaka kujiita hivyo wajiite tu.
“Muache tu huyo Dudu Baya aige hilo jina mimi sioni ubaya wake, unajua mimi siyo mtu wa kihivyo angalia hata Wasafi nao kwenye wimbo wao wa Tetema si wametumia vibwagizo vyangu na nimeona wako sawa tu.
“Mimi siyo mtu wa kumaindi mambo madogo kama hayo wewe waache waige tu,” alimaliza kusema Pierre
STORI: RICHARD BUKOS
Comments are closed.