The House of Favourite Newspapers

Pigo: Mama mzazi, mtoto wa dada yake Banza wafariki

0

 

Mama Banza

Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji mama mzazi wa Banza Stone, Bi. Khadija Masanja (kushoto) enzi za uhai wake. (Picha na Maktaba yetu)

PIGO limeikumba familia ya mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi, marehemu Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ marehemu Banza Stone baada ya kuondokewa na watu wawili wazito leo hii ambao ni mama mzazi na mtoto wa dada yake.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa aliyeanza kufariki dunia ni mtoto wa dada yake Banza Stone aitwaye Sozi Masanja ambaye alikuwa akiugua kwa siku kadhaa ambaye kafariki saa mbili asubuhi.

Masaa mawili baadaye mama mzazi wa Banza Stone, Bi. Khadija Masanja naye akafariki dunia kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni kutokana na mshituko wa kufiwa na binti yake.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. AMEN.

Leave A Reply