The House of Favourite Newspapers

Pikipiki ya Kwanza Global Kuondoka Leo

LEO ndiyo leo kwani msomaji mmoja wa Magazeti ya Global Publishers anatarajiwa kujishindia zawadi ya pikipiki ikiwa ni moja kati ya sehemu ya zawadi za promosheni ya Tusua na Global ambayo inaendeshwa na kampuni hiyo.

 

Leo Jumanne ndiyo itakuwa droo ya kwanza ya promosheni hiyo ambayo ilianza tangu wiki iliyopita ambapo msomaji wake atajishindia zawadi mbalimbali huku zoezi zima likitarajiwa kuonyesha mubashara kupitia Runinga ya Mtandaoni ya Global TV kuanzia saa 10:00 Jioni.

Akizungumza na Star Showbiz, Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho alisema kwamba, huu ni muda wa wasomaji kuanza kuvuna zawadi mbalimbali kupitia promosheni hiyo ya Tusua na Global ambapo kwa kuanza wanaanza na kutoa pikipiki mpya ambayo itatolewa leo.

 

“Tunaanza kwa kutoa pikipiki kwa msomaji wetu wa kwanza, Jumanne (leo) msomaji mmoja atapata zawadi hiyo tena zoezi zima litakuwa mubashara kwenye Runinga ya Mtandaoni ya Global TV saa 10 jioni.

“Hiyo itakuwa pikipiki ya kwanza kati ya 12 ambazo zipo, wanachotakiwa kukifanya wasomaji ni kununua zaidi tu magazeti pendwa ya kampuni yetu na kujiweka karibu zaidi na kushinda zawadi mbalimbali ambazo zipo.

 

“Tutakuwa tunatoa pikipiki kwa kila wiki na tumeamua kufanya hivyo kwa sababu tunarudisha fadhila kwa wasomaji wetu. Katika zawadi hizo hatutaacha hata sehemu ya jamii kwani kwa vijana kuna headphone za Beats By Dre huku kwa upande wa wakina mama kutakuwa na vyombo vya nyumbani lakini pia tutatoa jezi za timu ambazo zinashiriki Kombe la Dunia tena mshindi ndiye atachagua ni jezi gani ambayo anaitaka,” alisema Mrisho.

 

Kushiriki promosheni hii msomaji atatakiwa kununua Magazeti ya Championi, Amani, Ijumaa Wikienda, Spoti Xtra, Ijumaa, Uwazi na Risasi Mchanganyiko kisha kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili.

Star Showbiz.

Comments are closed.