The House of Favourite Newspapers

Pilau ya Nafaka na Nyama ya Kusaga

0

LEO ka­tika safu hii ya Mapishi ya Leo, tunaangalia jinsi ya kupika pilau ya nafaka na nyama ya kusaga kama waso­maji wengi mlivyoomba.

 

MAHITAJI

Mchele

Nyama ya kusaga

Nafaka uzipendazo kama mbaazi, maharage au njegere.

Vitunguu maji kata vi­pandevipande

Kitunguu saumu

Tangawizi

Mafuta ya kula

Bizari ya unga

Maji

Chumvi

 

KUTAYARISHA NA KUPIKA

Chambua mchele, uoshe na uloweke.

Chukua sufuria safi bandika jikoni acha lipate moto kisha mimina mafuta kiasi unacho­taka.

Mafuta yakishachemka mimina vitunguu maji na kaanga mpaka vibadilike rangi na kuwa kahawia.

Weka vitunguu saumu na tangawizi ambavyo vyote vimepondwa kisha kaanga kidogo.

Weka nyama ya kusaga, chumvi, bizari huku ukiende­lea kukaanga mpaka nyama iive.

Weka nafaka pekee na maji yake yamwage

Weka maji kidogo kisha koroga baada ya hapo weka mchele huku ukiendelea kukoroga.

Ukimaliza kukoroga funika pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukiko­rogoka kidogo (kama unavy­opika pilau ya kawaida).

Onja kama umeiva na umekauka maji vizuri, epua na pakua tayari kwa kuliwa.

Leave A Reply