The House of Favourite Newspapers

Pimbi: Marioo Kamfunika Harmonize Kimuziki, Amebaki Kutembelea Kiki ya Kajala

0
Pimbi msanii wa vichekesho nchini

MSANII wa vichekesho nchini anayefahamika kwa jina la Pimbi amesema kwa sasa kimuziki Marioo kamuacha mbali sana CEO wa Kondegang, Harmonize kwani kwa mwaka huu nyimbo ya Naogopa ndiyo nyimbo bora kuliko nyimbo yoyote ile.

 

Akiongea katika kipindi cha katambuga kinachorushwa na Global TV na Global Radio Pimbi amesema alichobaki nacho kwa sasa Harmonize ni kutembea na Kiki kwa kurudiana kimapenzi na Kajala Masanja lakini kimziki hana jipya.

Pimbi amesema Rayvanny ndiye msanii anayetumia pesa nyingi kwenye video zake

“Mpenzi wake Drama tui le inatengenezwa, iIle ni drama tu, yale magari unayoona pale sijui Kajala 1 sjui nini ile ni Show Room ipo Mwananyamala hapo ya mshokaji anaitwa Abdul, ye anachukua magari anaprint ana paki pale sijui ni konde Village anarekodi sjui anapiga picha na macameraman wake gari zinarudishwa.” Amesema Pimbi

Pimbi anadai kwa sasa Harmonize anatembelea kiki ya Kajala Masanja

Aidha amemuongelea Rayvanny kuwa ndiye msanii anayetumia pesa nyingi sana katika kutengeneza kazi zake ikiwemo kitendo cha kuchoma gari, kuchoma nyumba lakini kubwa kuliko ni kwamba Rayvanny amesitisha safari ya shirika la ndege lisifanye safari zake ili aweze kushoot video yake ndani ya ndege.

Leave A Reply