The House of Favourite Newspapers

Pique na Shakira Waburuzana Tena Mahakamani, Ni Kuhusu Ndege ya Kifahari ya Wawili hao

0
Pique na Shakira

MWANADADA mrembo ambaye pia ni mwanamuziki wa nyimbo za miondoko ya pop na rock Shakira na mpenzi wake wa zamani Gerard Pique wamejiingiza katika vita nyengine ya kisheria kuhusu ndege yao ya kifahari huku kukiwa na vita juu ya haki ya kuishi na watoto wao.

 

Mwimbaji huyo aliyetamba na kibao kikali cha Waka Waka na mchezaji huyo wa Barcelona walitangaza kutengana mwezi Juni mwaka huu jambo lililopelekea wawili hao kuajiri kampuni tofauti za uwakili ili kupambania haki za nani atakayekuwa na mamlaka ya kuishi na watoto wao wawili, Sasha na Milan.

Wawili hawa wamekuwa kwenye uhusiano kwa takribani miaka 11

Kupitia kampuni ya habari ya Marca imeripoti ya kwamba mwandishi wa habari Juan Carlos Ortega wa Prensa Libre alifichua kuwa wapenzi hao wa zamani wana mzozo mwingine juu ya ndege ya kibinafsi ya kifahari.

 

Ndege hiyo ya ukubwa wa kati ina thamani ya dola milioni 20 ambazo Shakira na Pique walinunua pamoja wakati wa uhusiano wao wa miaka 11.

Pique na Shakira wameingia kwenye mzozo juu ya Ndege ya kifahari

Ndege binafsi inayozungumziwa, Learjet 60XR, ina uwezo wa kuchukua hadi abiria 10 na ina vyumba viwili vya kulala, chumba cha kulia na sebule na TV pamoja na huduma zote za usafiri wa familia.

 

Ripoti hiyo inadokeza kwamba si Shakira wala Pique yupo tayari kuachana na ndege hiyo ya kifahari na wameripotiwa kukabidhi suala hilo kwa mawakili wao.

 

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply