The House of Favourite Newspapers

Pishi la aina moja ‘deile’ litamchosha mista!

0

chakula.jpgShoga zangu leo nimerudi tena na maneno kuntu shangingi mie, kwani nachoshwa na watu kuniambia wameachwa kila kukicha na hawajui nini sababu.

Hata hivyo, kila anayeniambia ameachwa huwa najaribu kumdadisi, si unajua tena shangingi ili kuwaeleza siri zangu na kunusuru ndoa zao nalazimika kuwachunguza kidogo ndiyo napata muafaka wa jinsi ya kuwafunda.

Kuna shost aliniambia ameachwa na wanaume watatu,  nikashangaa  hivi umeshashika uskani kwa nini unyang’anywe  na dereva mwingine, jikaze bibi fanya kila aina ya manjonjo ili kumtuliza umpendaye.

Utafanyaje sasa?

Si kila mwanaume anathamini mapenzi  ya chumbani tu, ingawa hata mapenzi hayo kwa wanaothamini pia huyakosa kisawasawa kwani  wanawake wengine hawajui  kubadili mlo hata huko chumbani, bila shaka watu wazima mnanielewa nisemacho.

Jitahidi kubadili mapishi ya mlo unaompa mwanaume chumbani, si kila siku pishi hilo hilo, akipata anayejua kukipika chakula vizuri utabaki kulia tu kwani nimefanya nini, hapo sasa! Naongelea chakula kinacholiwa chumbani.

Chakula halisi nacho kinahitaji ufundi

Kwa chakula kisicholiwa chumbani, nashauri pia kiangaliwe upya. Wapo wanawake wasiojua kukipika, utakuta mwanamke anampikia mumewe wali maharage kila siku, hana ratiba ya chakula na kama anajua kuweka mdalasini kwenye wali basi mume kila akipinduka ni wali wa mdalasini, ataacha kuchoka kweli?

Mashost buni chakula cha kumfurahisha mume ili hata akiwa ofisini au akiwa kwenye mihangaiko ya kusaka tonge, ajue kabisa atakuta chakula f’lani ameandaliwa.

Wanawake wengi wakishaolewa wanakuwa wavivu hata kubuni vitu vipya kwa sababu wanajua walishaipata ndoa, nawasihi mashosti zangu kuwa wabunifu, jikoni, sebuleni kwa chai hata chumbani kwa chakula cha usiku.

Kwa leo shangingi naishia hapa mengine tutaongea wiki ijayo.

Leave A Reply