Pistorius akutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake

1

Mwanariadha Oscar Pistorius ametiwa hatiani kwa kumuua mpenzi wake Reeva.

2 3

Pistorius atarudi kortini Januari mosi mwakani kusikiliza hukumu yake.

4

Mama mzazi wa Reeva, June Steenkamp (katikati) akifuatilia rufaa ya Oscar Pistorius leo.

5

Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.

Mahakama ya Rufaa nchini Afrika Kusini leo imemkuta na hatia mwanaraidha Oscar Pistorius kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Kutokana na uamuzi huo, mahakama imetengua uamuzi wa awali wa kuua bila kukusudia hivyo Pistorius atalazimika kurudi jela kutumikia kifungo.

Rufaa hiyo imesikilizwa mbele ya jopo la majaji watano ndani ya Mahakama Kuu ya Rufaa nchini Afrika Kusini ila mwanariadha huyo hakuwepo.

Pistorius, 29, anatakiwa kupanda kizimbani Januari mosi mwakani kusikiliza hukumu yake ambapo huenda akatumikia kifungo cha hadi miaka 15  kwa kosa hilo la kumuua Reeva.

Loading...

Toa comment