KOCHA wa Singida United, Hans van Der Pluijm amesema ubora wa washambuliaji, Ibrahim Ajibu wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba unaweza kufanya jambo lolote lisilotegemewa katika mchezo wa leo.
Ajibu anaongoza kwa kufunga Yanga akiwa na mabao matano huku Okwi akiongoza kwa ufungaji Simba na katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane, leo timu zao zinapambana kwenye Uwanja wa Uhuru.
Pluijm alililiambia gazeti hili kwamba; “Ajibu na Okwi wapo katika kiwango kizuri, hawa ndiyo wataamua matokeo lakini wanaweza kuchafua hali ya hewa kwa jambo lisilotarajiwa kutokea.”
Na Ibrahim Mussa