The House of Favourite Newspapers

Pluijm apata mfumo wa kuimaliza Simba mapema

0

PLUIJMKITAMBI

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Said Ally,Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ametamba kuendelea kutumia mfumo wa 4-4-2 katika mchezo dhidi ya Simba, kesho Jumamosi kutokana na kumpatia ushindi kila mara anapoutumia.

Yanga ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa wakiwa na pointi tisa na mabao tisa huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi zao tisa na mabao sita.

Yanga ilianza kutumia mfumo huo tangu kuanza kwa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambapo ilishinda 2-0 kisha 3-0 dhidi ya Prisons na 4-1 dhidi ya JKT Ruvu, hivyo Pluijm anaona una manufaa kwao.

Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana, amesema ataendelea kuutumia mfumo huo wa 4-4-2 katika mchezo wa Simba kutokana na kuona kuwa mbinu hiyo ya kiuchezaji imekuwa ikimpa matokeo mazuri katika kila mchezo.

“Naamini kuwa mchezo dhidi ya Simba utakuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu, hivyo tumejiandaa vya kutosha.“Tumepanga kuutumia mfumo wetu uleule wa 4-4-2 ambao umekuwa ukitupatia matokeo mazuri pale tunapokuwa tunautumia,” alisema Pluijm.

Leave A Reply