The House of Favourite Newspapers

Pluijm awaita Dida, Andrey Coutinho Dar

0

pluijm2.jpgNicodemus Jonas, Dar es Salaam

MDACHI wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amekaa chini na kutafakari matokeo yenye kutia wasiwasi kikosi chake kinapokuwa mkoani na kubadili gia.

Timu hiyo ilishikwa na Mwadui kwa kutoa sare ya mabao 2-2 mkoani Shinyanga, sasa ameamua kufungia kazi mechi za mikoani, wakati akijiandaa kuwakabili Mgambo JKT baadaye mwezi ujao.

Katika kuhakikisha hilo, Mdachi huyo ameagiza kikosi kuanza mazoezi kesho Alhamisi, Novemba 12, yaani mwezi mmoja kabla ya ligi kuendelea ili kuhakikisha timu hiyo inakuwa fiti.

Akizungumza na Champion Jumatano, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa benchi la ufundi liliamua programu kuanza siku hiyo na watakuwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, tayari kujiweka mguu sawa kuwakabili maafande wa JKT Mgambo kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, mchezo utakaopigwa Desemba 12, mwaka huu.

 “Mazoezi tutaanza Alhamisi wiki hii, ndiyo maamuzi ya benchi la ufundi, wale wote ambao hawapo kwenye majukumu ya timu za taifa, tutakuwa nao na kila mmoja anafahamu fika siku ya kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata,” alisema Hafidh.

Yanga itaanza mazoezi bila wachezaji wake wengi ambao wapo timu ya taifa, huku mastaa ambao wanatarajiwa kunogesha mazoezi hayo wakiwa ni Deogratius Munishi ‘Dida’ pamoja na Mbrazili, Andrey Coutinho.

Wakati Yanga wakiingia msituni, watani wao wa jadi, Simba wataanza kujikusanya Novemba 16, mwaka huu kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam ambao wao wataanza maandalizi Desemba 7, kuelekea mchezo huo utakaopigwa Desemba 12, mwaka huu.

Leave A Reply