The House of Favourite Newspapers

Pogba Afungiwa Miaka Minne Kutocheza Soka Kwa Tuhuma za Kutumia Dawa za Kusisimua Misuli

0

Mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Juventus ya Italia, Paul Pogba amefungiwa kutocheza soka kwa miaka minne baada ya vipimo kuonesha kuwa anatumia dawa za kusisimua misuli ambazo zimepigwa marufuku kwa wachezaji.

Kwa uamuzi huo, Pogba atakaa nje mpaka mwaka 2027 ambapo atakuwa na umri wa miaka 34.

Pogba alifanyiwa vipimo Agosti 2023 na kushindwa kuvuka kwenye kipimo cha DHEA ambapo vipimo vya damu vilionesha kuwa amekuwa akitumia dawa hizo.

Uamuzi huo umetolewa na Mamlaka ya Kuzuia Dawa za Kusisimua Misuli kwa Wachezaji nchini Italia, NADO.

Leave A Reply