Pogba Kuikosa Chelsea Ligi Kuu
PAUL Pogba anatarajiwa kuendelea kuwa nje kwa zaidi ya muda ambao alitarajiwa kuwa angerejea kutokana na kuwa majeruhi.
Taarifa hiyo inaweza kuwa siyo nzuri kwa mashabiki wa timu ya staa huyo, Manchester United, ambapo kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer pia alikiri Daniel James naye aliumia kiatika mchezo wa juzi dhidi ya Real Sociedad.
Pogba, amekosa mechi kadhaa tangu alipoumia katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Everton, Februari 6 ambapo anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Solskjaer pia aliwataja Edinson Cavani, Scott McTominay na Donny van de Beek kuwa wanaweza kuwa fi ti kwa ajili ya michezo ijayo ukianza ule wa Chelsea, kesho Jumapili, huku siku chache zijazo wakitarajiwa kukipiga dhidi ya Manchester City mechi zote zikiwa ni za Premier League.
Kuhusu Pogba, Ole alisema: “Paul bado ataendelea kuwa nje kwa wiki kadhaa.”