POLEPOLE AWAONYA CHADEMA KUPANGA VURUGU UKONGA – VIDEO

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekituhumua Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kupanga kufanya fujo katika Jimbo la Ukonga katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika keshokutwa Jumapili, Septemba 16, 2018.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole amesema tayari wamepata taarifa hizo na kwamba iwapo CCM nayo ingetaka kufanya hivyo isingeshindwa kwani wapo vijana imara wa UVCCM ambao wanaweza kupambana na vikundi hivyo ambavyo vimejipanga kuharibu uchaguzi huo.

 

Polepole ameviomba vyombo vya usalama vifanye kazi yake katika kuhakikisha hakuna tukio lolote baya ambalo litajitokeza siku hiyo ya Jumapili huku akisema CCM hakipo tayari kurumbana na vyama vingine vya siasa kwani chama hicho kinafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya katiba ya chama chao.

 

Katika Maelezo yake amesema kuwa chama hicho tayari kimejidhatiti kufanya kampeni za kweli katika chaguzi za marudio katika baadhi ya majimbo na amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Septemba 16 mwaka huu kwenye vituo vya kupigia kura ili watimize wajibu wao wa kisheria kuwachagua viongozi wao wanaowataka.

 

Aidha, amesema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeonyesha siasa chafu katika Jimbo la Ukonga hasa watu mbalimbali wa chama hicho wakitumia lugha fedheha.

 

Polepole ameongeza kwamba, CCM hakipo tayari kuona viongozi wake wakitumia lugha chafu katika chaguzi hizo za marudio na hata kama mmoja wanachama wake akiamua kwenda upinzani hawapo tayari kuanza kumshambulia hivyo siasa haipo hivyo na Watanzania waelewe kwamba CCM ndiyo chama pekee kinachofuata sheria ya nchi.

POLEPOLE: Chadema Wanafanya Fujo, Wanataka Kuvuruga Uchaguzi

Loading...

Toa comment