Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole Alipoongea na waandishi wa Habari.
KATIBU wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema ni vyema wananchi wakaanza kuwapuuza wanasiasa wa vyama vya upinzani wenye malengo ya kugeuza matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama hicho mtaa wa Lumumba, Polepole alisema kuwa CCM hakiwezi kushiriki au kusambaza taarifa za uongo kama vyama vya upinzani vinavyofanya ili kutafuta umaarufu usiokuwa na tija kwa lengo la kuleta uchochezi kwa wananchi.
Matamko mbalimbali yamekuwa yakitolewa na vyama mbalimbali kwamba taifa limekumbwa na baa la njaa.
“Tupuuze maneno ya wanasiasa, aliye na mamlaka ya kutangaza baa la njaa nchini ni rais peke yake hivyo ni vyema wanasiasa hao wakajua kuwa Tanzania haijafikia kiwango hicho cha baa la njaa. Chakula kipo na kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ambayo yana upungufu wa chakula,” alisema.
Vilevile alisema sera ya CCM ni kujitegemea, kama chama kinachoongoza dola, hakijafikia hatua ya watu kukosa chakula nchini.
- Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole akizungumza na wanahabari jijini Dar leo.
- Wanahabari waliokuwa katika mkutano ulioitishwa na Polepole wakichukua matukio mbalimbali
Kwa taarifa kamili tembelea www.globaltvtz.com
Na Denis Mtima/GPL
Comments are closed.