The House of Favourite Newspapers

Polisi Arekodiwa Akimkanyaga Kichwani Mtu Kwenye Uwanja wa Ndege

Afisa wa polisi amerekodiwa akimpiga akimkanyaga kumpiga kichwani mwanamume alikuwa amelala chini kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester nchini Uingereza.

Afisa huyo wa kiume aliyevalia sare anaonekana akiwa ameshikilia silaha aina ya Taser ( kifaa kinachotumika kujilinda bila kusabaisha madhara) juu ya mwanaume huyo, ambaye amelala kifudifudi, kabla ya kumpiga mara mbili huku maafisa wengine wakiwapigia kelele watazamaji , katika video iliyosambazwa sana mtandaoni.

Polisi wa Greater Manchester (GMP) walisema maafisa wa bunduki walishambuliwa walipokuwa wakijaribu kumkamata mtu kufuatia mapigano yaliyotokea kwenye uwanja wa ndege siku ya Jumanne.

Hasira kuhusu video hiyo imeendelea kuongezekana mamia ya watu waliandamana nje ya kituo cha polisi huko Rochdale, Greater Manchester Jumatano kulaani kitendo hicho.

PESA NDEFU ALIYOLIPWA DR CHENI HARUSI ya MTOTO wa RAIS MWINYI – “WATOTO wa BAKHRESSA WALIKUWEPO”…