The House of Favourite Newspapers

Polisi auawa akimuokoa bintiye

0

MAUAJI YA POLISI (6)

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

DAR ES SALAAM

ASKARI Polisi wa Kituo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wachuku Lotson Mwaipasi (51) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi, wakati akijaribu kumsaidia binti yake aliyekuwa akitaka kuporwa dukani huko Bunju, nje kidogo ya jiji wiki iliyopita.

MAUAJI YA POLISI (3)Kwa mujibu wa majirani wa marehemu, alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa bintiye huyo aliyekuwa akipigwa makofi huku akilazimishwa kutoa fedha, lakini alipofika na kuanza kupambana na mtu huyo, jambazi mwingine aliyekuwa pembeni alichomoa bastola na kumpiga risasi iliyomuua papo hapo.

MAUAJI YA POLISI (5)Mwili wa marehgemu ukiandaliwa kwa ajili ya kuagwa.

Inadaiwa kuwa hiyo ni mara ya pili kwa askari huyo kuvamiwa dukani kwake ndani ya muda mfupi, kwani Agosti mwaka huu, watu wanaodhaniwa kuwa wezi walifika na kutaka kupora.

MAUAJI YA POLISI (1)Marehemu Wachuku Lotson Mwaipasi, enzi za uhai wake.

Inadaiwa kuwa kabla ya mauaji hayo kutekelezwa na wenyewe kutokomea kusikojulikana, majambazi hao walivamia maduka mengine na kupora fedha.

MAUAJI YA POLISI (7)Mtoto wa marehemu akifarijiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema msako mkali unaendelea kuhakikisha wauaji hao wanatiwa mbaroni.

Alisema idara ya upelelezi itafanya kazi yake kwa haraka ili kuwanasa watu hao huku akitaka kupewa maendeleo ya msako huo kila mara.

MAUAJI YA POLISI (2)Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyehudhuria msiba wa askari huyo, alisema akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, hakubaliani na mauaji hayo hivyo akataka polisi kuongeza juhudi katika kuwatafuta wauaji hao.

MAUAJI YA POLISI (4)DC Makonda akitoa pole kwa wafiwa na Jeshi la Polisi.

Marehemu Mwaipasi alizikwa nyumbani kwao mkoani Mbeya Novemba 4, mwaka huu.

Leave A Reply