The House of Favourite Newspapers

POLISI Dar Yanasa Majambazi, Yaahidi Kuimarisha Amani Uchaguzi Ukonga

Jeshi la Polisi litaimarisha ulinzi siku ya uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 16.09.2018 wa ubunge jimbo la Ukonga na udiwani kata ya Vingunguti ili kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika katika misingi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

 

Rai ya Jeshi la Polisi kwa wananchi ni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazo elekezwa siku hiyo na wahusika wa uchaguzi bila kuleta vurugu au wao kuwa chanzo cha vurugu.

 

Katika kila kituo cha kupigia kura kutakuwa na askari wa vikosi mbalimbali, wakifanya doria kila sehemu wakiongozwa na askari maalumu wa kikosi cha kutuliza ghasia.

 

Jeshi halitasita kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi chochote chenye nia ya kufanya vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na kanuni au sheria ya uchaguzi.

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: KUKAMATWA KWA BASTOLA TATU NA RISASI 50, NA WATUHUMIWA 8 WANAOPORA PIKIPIKI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 08 /09/ 2018 majira ya saa 20:30hrs usiku huko maeneo ya Tandika askari wakiwa doria walitilia mashaka pikipiki aina ya TVS KING rangi nyekundu ambayo haikufahamika namba zake mara moja ikiwa na watu(2), Watu hao walipogundua wanafuatiliwa na Polisi walikimbiza pikipiki yao kwa mwendokasi huku wakirusha risasi hewani kuelekea maeneo ya Shule ya Sekondari Tandika. Aidha katika purukushani hizo watu hao walitupa bastola No. DAA 317079 aina ya Berreta ikiwa na risasi moja ndani ya magazine.
Polisi wanaendelea na msako mkali kuwatafuta ili kubaini mtandao mzima na matukio waliyowahi kuyafanya. Katika tukio lingine
Mnamo tarehe 08/09/2018 majira ya saa 19:30 hrs usiku huko maeneo ya Chanika mtu mmoja aitwaye HASSANI S/O MAULID mkazi wa Gongo la mboto, aliporwa bajaji No. MC 536 BGT aliyokuwa akiendesha. Kabla ya tukio hilo dereva huyo wa bajaji alikodiwa na wanawake wawili toka Chanika kuwapeleka Mvuti na walipofika eneo la kwa Baja ghafla gari aina ya ALPHARD T.474 DHS rangi nyeupe vioo vikiwa tinted iliwazuia kwa mbele, Mtu mmoja alishuka na kumtishia silaha dereva huyo na hatimaye kumnyang’anya bajaji na kutokomea nayo kusikojulikana.
Jeshi la Polisi lilipata taarifa na kuanza msako mkali hatimaye kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ARTHAR s/o KASILILIKO na watuhumiwa wengine (7) akiwemo mwanamke mmoja umbali wa kilomita mbili toka eneo la tukio, upekuzi wa awali ulifanyika kwa mtuhumiwa wa kwanza na kukutwa na Bastola moja aina ya BERRETA yenye namba H44978Y, ikiwa na magazine 2 na risasi (13) kila moja ndani ya magazine na boksi moja likiwa na risasi(21) na kufanya jumla ya risasi 47.
Aidha msako mkali unaendelea kuitafuta bajaji hiyo huku watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watapelekwa mahakamani upelelezi utakapokamilika. TUKIO LA 3, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 27 August 2018 majira ya 13:00 hrs huko maeneo ya Nguvu kazi Chanika lilipokea taarifa kutoka kwa mmiliki mmoja wa nyumba kuwa kuna Bastola aina ya Browning iliyofutwa namba ikiwa na risasi moja ndani ya magazine kwenye chumba cha mpangaji wake.
Upelelezi unaendelea ili kumbaini mmiliki wa silaha hiyo. POLISI KANDA MAALUM DSM KUIMARISHA ULINZI WAKATI WA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA UKONGA NA UDIWANI KATA YA VINGUNGUTI Jeshi la Polisi litaimarisha ulinzi siku ya uchaguzi mdogo utakaofanyika tarehe 16.09.2018 wa ubunge jimbo la Ukonga na udiwani kata ya Vingunguti ili kuhakikisha mchakato wote wa masuala ya uchaguzi unafanyika katika misingi ya sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.
Napenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Jeshi la Polisi limejiandaa vizuri kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi huo na kuwaonya waliopanga kufanya vurugu kuwa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Rai ya Jeshi la Polisi kwa wananchi ni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazo elekezwa siku hiyo na wahusika wa uchaguzi bila kuleta vurugu au wao kuwa chanzo cha vurugu.
Katika kila kituo cha kupigia kura kutakuwa na askari wa vikosi mbalimbali, wakifanya doria kila sehemu wakiongozwa na askari maalumu wa kikosi cha kutuliza ghasia. Jeshi halitasita kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi chochote chenye nia ya kufanya vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na kanuni au sheria ya uchaguzi. L.B.
MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
14.09.2018

Comments are closed.