Polisi DSM ‘Walivyowaua’ Majambazi Sugu Ukonga! – Video

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wawili na kukamata silaha moja aina ya Chinese Pistol ikiwa na risasi tatu na maganda manne ya risasi ya bastola hiyo.

 

Akizungumza na wanahabari mapema leo Februari 11, Kamanda wa kanda Maalum ya DSM, Lazaro Mambosasa, amesema Mnamo Februari 9, mwaka huu majira ya saa tatu usiku maeneo ya Ukongo kikosi kazi cha kupambana na wahalifu kilipataa taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna pikipiki ambayo haina namba za usajili imeonekana maeneo ya Pugu, hivyo kikosi hicho kikafunga safari mpaka maeneo hayo.

 

Wakiwa njiani kukaribia eneo hilo walikutana na pikipiki hiyo na kumuamuru dereva aliyekuwa akiendesha pikipiki hiyo kusimama lakini aliakadi na kuanza kuwashambulia askari kwa risasi ambao nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi vibaya ambapo walifariki wakiwa njiani kuelekea hospitali.

TAZAMA MAMBOSASA AKIFUNGUKA

Toa comment