The House of Favourite Newspapers

Polisi Kanda Maalum DSM Yamnasa Furaha wa Kuposti Picha Chafu Mtandaoni

0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la mauaji ya watu wawili, Japhari Mwinyimvua (40) mlinzi  na Richard Nonyo (65) baba mzazi wa mtu anayedaiwa ni mganga wa kienyeji wa eneo hilo.
Tukio hilo limetokea Aprili 21, 2024 majira  ya saa 3 asubuhi maeneo ya Kigogo fresh, Pugu, Ilala ambapo mlinzi huyo alikutwa ameshambuliwa na baadae kupoteza maisha. Hata hivyo katika mtiririko huo kundi la watu lilimshambulia baba mzazi wa mganga huyo na baadae akapoteza maisha wakimtuhumu mtoto wake kuhusika na kifo cha mlinzi huyo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wanachunguza  kwa kasi tukio hilo na wahusika wote wa tukio hili watakamatwa haraka iwezekanavyo  na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria .
Katika hatua nyingne, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Furaha Dominick Jacobo (32) mkazi wa Masaki na Mustafa Kihenga (28) mkazi wa Mwenge TRA kwa tuhuma za  uhalifu wa kimtandao kwa kusambaza picha chafu za video za watu zisizo na maadili kwa lengo la  kujipatia fedha kwa vitisho.
Watuhumiwa hawa wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo kujibu tuhuma zanazowakabili.
Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO – SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Leave A Reply