testiingg
The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Polisi Mwanza lakamata wahalifu 264, RPC Atoa onyo

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza baada ya  kufanya misako na doria mbalimbali na limefanikiwa kukamata watuhumiwa 264 wa makosa mbalimbali ya uhalifu katika kipindi cha siku 13 kuanzia tarehe 01, Aprili hadi 13, Aprili mwaka huu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Tarehe 13.04.2023 muda wa saa 02:00 huko katika Kata ya Magu mjini, Tarafa na Wilaya ya Magu, katika barabara ya Mwanza/Musoma, Gari namba T.826 DKK aina ya Mazda Primas, mali ya Beatus Francis @Chiganga, lilikamatwa likiwa na viroba tisa (9) vya mirungi inayokadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kiloagram 70. Awali Gari hilo kabla ya kukamatwa liligonga kizuizi cha magari na kupoteza uelekeo kisha kugonga mti, baada ya tukio hilo dereva alikimbia na kwenda kusiko julikana.

Baada ya upekuzi katika Gari hilo Askari walikuta viroba tisa vya mirungi na kufanikiwa kuvifikisha kituo cha Polisi Magu pamoja na Gari hilo lililokuwa limepata uharibifu wa kupasuka tairi tatu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka dereva wa Gari hilo kwa tuhuma za kosa la kusafirisha dawa hizo za kulevya aina ya mirungi ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kupitia kwa kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa  Wilbrod  Mutafungwa- SACP  amesema jeshi hilo linaendelea kutoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa wepesi na haraka.

Leave A Reply