Polisi: Mauaji ya Pope Smoke ni Mpango
JUMATANO ya wiki iliyopita, ulimwengu wa Hip Hop ulimpoteza moja ya marapa chipukizi waliotabiriwa makubwa, Pope Smoke ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Hollywood Hills huko Los Angeles Marekani.
Taarifa za mwanzo zilisema kuwa mauaji ya rapa huyo yalitokana na uvamizi wa majambazi waliokuwa na lengo la kupora mali nyumbani kwa msanii huyo, lakini taarifa mpya zilizotoka juzikati zimesema kuwa tukio hilo halikuwa la uvamizi wala uporaji bali ni mpango uliosukwa wa kumuua rapa huyo.
“Tumefanya uchunguzi katika kamera za ulinzi, tumegundua ule haukuwa uvamizi bali ni mpango hasa uliosukwa na kudhamiria kuchukua maisha ya Smoke, taarifa zaidi zitatoka baada ya uchunguzi kukamilika,” kilisema chanzo.
Qaissy Mohamedy, Risasi