Polisi Tz, Msumbiji Kufanya Oparesheni Pamoja

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji, Bernadino Rafael, wamekubaliana kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na kikundi cha watu wanaofanya uhalifu katika maeneo ya vijiji vya mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili.

 

Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati wakuu hao walipokutana mkoani Mtwara na kufanya kikao-kazi cha ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili ambapo wote kwa pamoja wamesema wataendelea kuishirikisha jamii ili  kupata taarifa zitakazosaidia kukomesha mtandao huo wa kihalifu.

Toa comment