Polisi Wafichua Miili ya Watu Ishirini Iliyokaushwa,Majirani Watoa Neno

POLISI katika mji wa Benin katika Jimbo la Edo kusini mwa Nigeria wanawashikilia watu watatu kutokana na kugundulika kwa miili ishirini (20) katika eneo linalodhaniwa ni takatifu.
Msemaji wa Polisi, Chidi Nwabuzor,alieleza hayo alipokuwa akihojiwa na BBC ya kwamba maiti 15 za wanaume, wanawake watatu na watoto wawili zimegundulika. Japo bado haijajulikana ni kwa muda gani m,aiti hizo zimekua katika eneo hilo.

Msemaji huyo wa Polisi aliongeza kuwa maafisa wa Polisi wenye silaha na walinzi wa eneo walivamia jengo hilo lililopo nje tu ya mji kufuatia taarifa waliyopewa kwa siri.
Kupatikana kwa miili hiyo umewashitua na kuwaogopesha watu nchini Nigeria na wakazi wa eneo hilo wanasema wametishwa mno na tukio hilo.

Wengi wao wanauliza ni kwa namna gani miili hiyo iliweza kufichwa pale bila majirani na watu wanaozunguka eneo hilo kutokufahamu tukio hilo.
Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao