The House of Favourite Newspapers

POLISI WAFUNGUKA KUMSHUSHIA KIPIGO ‘HEVI’ DEREVA WA FUSO

JESHI la Polisi mkoani Songwe limeeleza sababu ya askari wa usalama barabarani kumshambulia dereva kwa kipigo kuwa alitumia lugha ya matusi na kutotii amri ambayo ilimtaka atoe ushirikiano kwa askari hao waliyokuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na maofisa wa Sumatra.

 

Hayo yamesemwa leo  na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, Yusuph Sarungi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, Januari 14, 2019 ambapo amesema tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi majira ya saa 2:30 asubuhi katika eneo la Transforma, Tunduma, wilayani Momba wakati askari hao na Sumatra wakiwa kwenye ukaguzi wa magari mbalimbali eneo hilo.

 

Sarungi  amesema dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Mawazo Jairos (29) mkazi wa Mbeya, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Mistubishi Fuso lenye namba za usajili T842 AAC, baada ya kusimamishwa alianza kutoa lugha za kashifa na matusi kwa askari na maofisa wa Sumatra na kuondoa gari bila ya kuruhusiwa kwa kupitia barabara ya vumbi hali iliyolazimu askari hao kumfukuzia na kumkamatia eneo la Makambini kisha kumzuia tena.

“Dereva huyo aliteremka kwenye gari kwa jazba huku akiendelea kutoa matusi na kumshambulia askari ambapo hata hivyo askari hao walifanikiwa kumdhibiti hali iliyofanya apige kelele kuomba msaada. Wananchi walifika lakini wakati wanamsaidia, alifanikiwa kuwatoka na kwenda kwenye gari kisha kuchukua panga kuwatishia askari hao, alifanikiwa kuondoa gari eneo la tukio hadi alipokamatwa tena katika Mji wa Vwawa,” alisema Sarungi.

 

Aidha, Kamanda Sarungi amesema kuwa askari polisi hao walikuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi kwa kumdhibiti dereva huyo kwa vile sheria inawaruhusu kutumia nguvu za kadri ili kumdhibiti mhalifulicha ya askari mmoja kujeruhiwa vibaya.

 

Sarungi ameongeza kuwa, Mawazo atafikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma za makosa mbalimbali aliyofanya, ambapo kosa la kwanza kumjeruhi askari, kosa la pili kuzuia askari na Maofisa wa SUMATRA kufanya kazi yao.

 

INASIKITISHA: Aungua Moto Bila Kujua Apoteza Fahamu Siku 3!

 

View this post on Instagram

 

Video inayosambaa mitandaoni ikiwaonyesha askari wa usalama barabarani wakimshambulia kwa kipigo dereva wa fuso huko Songwe.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

 

View this post on Instagram

 

Video inayosambaa mitandaoni ikiwaonyesha askari wa usalama barabarani wakimshambulia kwa kipigo dereva wa fuso huko Songwe.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.