Polisi wamemwagwa kwa wingi mitaani ambapo vituo vya treni za chini ya ardhi pamoja na angalau shule moja vitafungwa kutokana na wasiwasi wa usalama wakati Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini itakapotoa uamuzi wa kumwondoa au kumrudisha madarakani Rais Yoon Suk Yeol aliyepigwa kura ya kutokuwa na imani.
Hatima ya kisiasa ya Yoon ipo mashakani baada ya amri yake ya kijeshi ya muda mfupi ya Desemba 3 kusababisha kuondolewa kwake madarakani na kukumbwa na mashtaka tofauti ya jinai.
Uamuzi wa kumwondoa madarakani unatarajiwa kutolewa hivi karibuni wiki hii, na wafuasi na wapinzani wa Yoon wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi, huku maandamano ya hivi karibuni yakikusanya makumi ya maelfu ya watu.
Maafisa wa polisi wamesema wanaweza kutumia maji ya kuwasha au virungu iwapo kutatokea vurugu kama zile zilizotokea wakati wa fujo za wafuasi wa Yoon katika jengo la mahakama mwezi Januari, Lee aliongeza.